MAJAMBAZI WALIVUNJA na
kuingia katika nyumba ya aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez
viungani mwa mji wa Bueno Aires nchini Argentina siku ya Jumapili na kuiba
wakati nyota huyo alipokuwa nchini Uruguay kufunga ndoa.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa
Tevez hakuwasilisha ripoti kwa polisi kuhusu wizi huo hivyobasi haijulikani ni
nini kilichoibiwa.
Tevez na mke wake tayari
wameondoka na kuelekea Mexico kwa fungate yao.
Polisi wanasema kwamba waligundua
kuhusu wizi huo siku ya Jumanne baada ya kuwaona wanahabari wamekusanyika nje
ya nyumba hiyo ya nyota huyo wa Argentina.
Wanasema kuwa wezi wengi
waliingia katika nyumba hiyo ambayo Tevez na familia yake walikuwa wamekodi
huku wakisubiri nyumba yao ambayo ilikuwa inafanyiwa ukarabati.
Inadaiwa wezi hao waliingia
nyumba hiyo kupitia eneo ambalo ukarabati huo ulikuwa ukifanywa.
Baada ya Tevez kuarifiwa kuhusu
wizi huo, alirudi nyumbani kwake kwa helikopta .
Aliukuta mlango wa nyumba yake
uko wazi huku vitu vikiwa vimepekuliwa.
Tevez baadaye alisafiri kuelekea
Mexico kama alivyopanga kwa fungate yake na mpenziwe wa utotoni Vanesa Masilla.
Wawili hao waliokutana wakiwa na
umri wa miaka 13 na ambao wana wasichana wawili, walifunga ndoa katika sherehe
ya kawaida siku ya Ahamisi mjini Bueno Aires.

No comments:
Post a Comment