KWANZA KABISA ningependa
nichukue nafasi hii kukupongeza kwa mafanikio makubwa ya single yako ya Muziki,
kiukweli ni nyimbo ambayo kwa mwaka 2016 imekuwa gumzo na japokuwa sina data za
kutosha naweza thubutu kusema inaweza kuwa ni ndio nyimbo iliyosikilizwa zaidi
na kuwafikia watu wengi sana kwa muda mfupi toka ilipotoka.
Lengo kubwa la mimi
kukuandikia “open letter” hii ni kujaribu kuelezea ideas zangu ambazo nahisi
zinaweza kukupa “support” zaidi kwenye safari yako ya kuwa mmoja wa wasanii
wakubwa ndani na nje ya nchi yetu hasa ikizingatiwa ya kwamba muziki wetu upo
kwenye “direction” nzuri sana ya kuwa mkubwa zaidi barani Afrika.
Pili, haya ni mambo
ambayo nimekuwa nikiyawaza kwa muda mrefu zaidi juu wa wasanii wa muziki wa
hapa Bongo na kuyatafakari kwanini hayafanyiwi kazi na wadau wa muziki au hata
kama yanafanyiwa kazi mbona “impact” yake hatuioni kivile?
Disclaimer: Naandika
haya mambo kama mawazo tu kutokana na experience yangu ya biashara zangu na pia
kupitia experience ya kuangalia watu wengine wanafanyeje. “I’m not claiming to
be an expert” kwenye music or kwenye biashara. Kuna uwezekano mkubwa vitu
nitakavyosema hapa visiwe applicable kwako kutokana sababu zako binafsi au
plans zako za kimuziki. Na wala sitoi guarantee yoyote kuwa mambo haya
yatafanya kazi kama ninavyosema. “They are just ideas that you can choose to
work on them or trash them”
Tukiachana na
‘disclaimer’ hapo juu, vitu vitatu tu ambavyo ningependa kuvielezea leo ni
1. Branding
2. Monetization strategies
3. Self-promotion
1. Branding
Kwanza kabla ya
kuelezea kuhusu branding naomba niseme kuwa kaka mkubwa umetoboa. You are a
star now, maana sio kwa attention na positive response ambayo Muziki imepata.
Kutoka kwako nakufananisha na kipindi ambapo Wiz Khalifa wakati anaanza muziki.
Alitoa track chache ambazo zilisikika sikika kisela then baadaye akatoa “Teach
U to Fly” na “Say yeah” ambazo zilifanya vizuri zaidi kabla ya kutoa “Black and
Yellow” ambayo ilibadilisha kila kitu kwake.
Tofauti na sisi
wabongo mbele watu sababu wanajua muziki zaidi na wanajua biashara, once
wakitoa kitu kikakubalika na jamii huwa ‘immediately’ wanajua nini cha kufanya
ili kuji-brand kama wasanii wakubwa kuendana na soko. Na branding nayoingelea
hapa sio branding ya lifestyle na mavazi au level za bata, ni branding ya kuji
– associate wewe na muziki wako kwamba watu wajue Darassa ni nani, na ndo yule
aliyeimba ule wimbo wa muziki hata wakiamshwa usiku wa manane.
Maana nachokiona ni
kwamba wimbo huu umekuwa mkubwa sana, lakini nachojiuliza ni, Je? Jina lako
linakuwa sambamba na wimbo? Watu wanakujua Darassa kama Darassa? Na kila
wakiusikiliza / kuutazama wimbo YouTube wanakumbuka jina la mwanamuziki nyuma
yake?
Hii ishu niliiwaza
sana pia wakati Man Fongo katoa wimbo wake wa ‘Hainaga Ushemeji’, maana ule
wimbo kwakweli kama ni kutusua Man Fongo alitusua ila Je, watu wamemjua Man
Fongo kama Man Fongo? Au wamebaki kukumbuka tu phrase ya “hainaga ushemeji” na
kumsahau Man Fongo? Na vipi kesho akitoa/ukitoa wimbo mwingine watu
watalikumbuka jina lako hata kama wimbo sio mkali kama huu na hauna a catchy
phrase kali kama “hainaga ushemeji” au “acha maneno weka mziki”?
Moja ya case study
yangu nzuri sana ya hii type ya branding ni kwa kuangalia na kujifunza nini
Soulja Boy alikifanya alipotoboa na wimbo wake wa “Crank That” mwaka 2007 au
juzi hapa Desiigner alipotoa Panda au T-pain alipotoboa na matumizi yake ya
autotune kwenye nyimbo.
Ni kweli hatuwezi
kujilinganisha na “resources” walizonazo wenzetu lakini tunaweza kujifunza
kutoa kwao. Ingawa crank dance zilikuwepo before, Soulja Boy aliweza kuji-brand
na crank kiasi kwamba mpaka leo mtu akiwaza crank dance lazima amkumbe Soulja
Boy kwa njia moja ama nyingine, the same applies to T-Pain na auto-tune au
“Panda” na “Desiigner”
2. Monetization strategies
Najua bado ni changamoto
hapa nchini kwa wasanii kunufaika moja kwa moja kupitia single zao wanazotoa
kwa njia mbadala tofauti na show na caller tunes ambazo wengi wenu ndo mmeanza
kunufaika siku za karibuni. Lakini pamoja na chagamoto hizi bado mi naona bado
kuna opportunities nyingi sana ambazo wasanii wanaweza kuzitumia ili
wanufaikezaidi na singles zao na kuacha kutugemea shows tu.
Mfano, kupitia hii nyimbo yako ya Muziki, baadhi ya vitu ambavyo
management yako ingewezza kuvifanya ili wewe ufaidike zaidi ni pamoja na hivi
vifuatavyo:
1. Public Sponsored shows
Hizi ni shows ambazo
management yako inaweza kuzindaa kwa ajili ya public lakini zikadhaminiwa na
makampuni machache. Tofauti na ilivyo sasa ambako makampuni ndo yanandaa show
na kukuita wewe, unaweza ukaandaa wewe show na kuyafuta makampuni kuyaambia
kuwa utatangaza bidhaa zao kwenye show yako kwa gharama fulani ambayo sio kubwa
na wenyewe wanaweza kuja kuuza/kutangaza bidhaa zao hapo maana mkusanyiko
utakuwepo maana ni uhakika watu wakakuja kusikiliza muziki.
Ukipata hata kampuni
10 zikakupa milioni 2 -3 ukafanya hii routine kwa mikoa mitano mikubwa, nadhani
kuna number zitaongezeka benki a pia itakusaidia kukuza jina lako kwa
mashabiki.
Na sio lazima utafute makampuni makubwa kama Tigo au Vodacom, zipo mid-sized
companies ambazo zinazoweza kutoa hela hiyo bila shida yoyote au a long
procedure itakayokufanya ushindwe ku-execute plan yako on time.
2. Mauzo ya branded Tshirts/kofia
Hili lipo wazi nadhani
na naona kuna wasanii wanafanya tayari. Kuprint t-shirt na kofia sio kazi, tena
unaweza ukaagiza mzigo fasta tu China ukaja ndani ya wiki. Uzuri kwa wewe wimbo
wako una catch phrase safi kabisa “Acha maneno, weka muziki” . I’m sure watu
kibao watachangamkia t-shirt zako na kofia ambazo unaweza kuzioua kupitia
kwenye shows zako hizo za wazi au hata kupitia mtandao
3. Mauzo ya branded accessories
Hii pia ni kama mauzo
ya t-shirts na kofia tu. Unaweza print vitu kama car stickers, stickers za boda
boda, bajaji na ntingine kibao tu watu wazinunue na ukauza kwa staili kama ya
Tshirts au kofia
4. Youtube Video
Nimekuwa nikifuatilia
channel yako ya Youtube na sioni kama unaitumia effective kukuingiiza kipato
cha ziada. Angaliana jifunze kupitia channel ya Diamond au wasanii wengine huko
mbele. Vitu kama behind the scenes, interviews, funny clips zako, studio
sessions, tours n.k vinaweza kuwa opportunity ya wewe kutengeneza passive
income nzuri tu. There is a reason why wasanii wakubwa wa nje wanakuwa na
personal videographer wao au ptotographer na wanapost post vitu Youtube. Sio kwa
ajili ya fans tu. Kuna hela pia nzuri sana ya kutengeneza hapo
5. Online Store /website
Unaweza kuset up
online store au website yako ambayo watu wanaweza kununua vitu vilivyotajwa
hapo juu kwa urahisi zaidi na pia inakuwa ni njia moja ya ku-control wa mauzo
yako halisi na fake toka kwa watu wanao duplicate kazi zako. Yote haya na mambo
mengine mengi ambayo sijayataja ni mambo ambayo management yako inaweza
kujipanga na kuyafanyia kazi (kama haijaanza kuyafanyia kazi sasa hivi)
taratibu kuanzia kwenye wimbo huu wa muziki na nyimbo zake nyingine zinazokuja
3. Self-Promotion
Kitu cha tatu na cha
mwisho ambacho ningependa kuki-adress ni self-promotion.
Nimejaribu kupitia social media accounts zako kuangalia nini unafanya na naona
bado sula la self-promotion yako inabidi uli-upgrade kidogo kama inawezekana.
Facebook : page likes – 315 tu
Twitter : followers 952 tu
Instagram : folowers 818 tu
Youtube : 22,842
Kwa muda huu ambapo
Muziki ndo habari ya mjini hizi number zingetakiwa ziwe zinakuwa sawa na idadi
ya watu wanaosikiliza muziki, maana hawa fans ndo listeners/viewers wa ngoma
yako ya kesho. Wakiwa wengi zaidi ndo track yako inavyosambaa kwa haraka zaidi
na kuwafikia watu wengi zaidi. Kama unazi-manage mwenyewe hizi accounts tafuta
hata dogo basi wa kuzi-keep busy on the side ukiwa wewe una mambo mengine ya
kufanya. I’m sure huwezi shindwa ku-afford kumlipa hata elfu 50 kwa wiki.
Angalia mfano wa
social media accounts za kina Chris brown kuanzia Facebook mpaka Instagram
utaona jinsi wenzetu wapo serious na self-promotion. Na hili sio kwako tuu,
nimekuwa nikiangalia accounts za wasanii kibao hapa bongo wengi social media
zao ni majungu tu na vijembe badala ya kutumia kama platform za kuwaingizia
kipato.
Ukitazama wenzetu
especially kwenye situation kama hizi wanapokuwa kwenye chat utafurahi jinsi
walivyo serious na self-promotion. Kuna vitu vidogo unaweza fanya ilikuwa-
incentives mashabiki waondelee kuiongelea ngoma yako zaidi. Mfano mwingine
mzuri ni Tekno miles alipotoa track yake ya“Pana”, kama ulimfuatilia kidogo
nadhani uli-notice jinsi gani alivyokuwa serious ku-promote ngoma yake mpya
hiyo maana alijua ni hit song na inahitaji kupushiwa zaidi.
Conclusion
Kama nilivyosema hapo
awali, lengo langu ni kujaribu kuweka wazi mawazo yangu ambayo naamini yanaweza
kuwa ni changamoto kwako na kwa wasanii wengine watakaoweza kupata nafasi ya
kutoboa kama wewe. Nachokiamini mwisho wa siku muziki huu unaoufanya lazima ukulipe
kwa namna moja au nyingine ndo maana umekomaa miaka yoye hii kufika hapo ulipo.
Na mimi kama mtanzania mwenye kujivunia kazi nzuri za watanzania wenzangu sina
budi ku-support kizuri kutoka nyumbani.
Inawezekana
niliyoyasema hapo tayari mnayafanyia kazi au yapo kwenye pipeline ila all in
all I had to say something maana Muziki imekuwa ni ngoma kubwa sana na
nimefurahi pia maana imezinyamazisha zile pande kubwa mbili zenye maneno mengi
sana mtandaoni na sasa hivi wamenyamaza wanaweka muziki tu.
I wish you get the best in your career and I wish utoe ngoma
kali zaidi ya muziki.
Acha maneno, weka muziki